Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yopa
Yoshua 19 : 46
46 Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 16
16 ① nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
Ezra 3 : 7
7 ⑥ Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
Yona 1 : 3
3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.
Matendo 9 : 43
43 Basi Petro akakaa siku kadhaa huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.
Matendo 10 : 18
18 wakaita; wakauliza kama Simoni aitwaye Petro anakaa humo.
Leave a Reply