Biblia inasema nini kuhusu Yohana – Mistari yote ya Biblia kuhusu Yohana

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yohana

2 Wafalme 25 : 24
24 Na Gedalia akawaapia wao na watu wao, akawaambia, Msiogope kwa ajili ya watumishi wa Wakaldayo; kaeni katika nchi; mkamtumikie mfalme wa Babeli; itakuwa vyema kwenu.

Yeremia 40 : 16
16 Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohana, mwana wa Karea, Usilitende jambo hili, maana unamsingizia Ishmaeli.

Yeremia 41 : 15
15 ③ Lakini Ishmaeli, mwana wa Nethania, akatoroka pamoja na watu wanane, Yohana asimpate, akawaendea wana wa Amoni.

Yeremia 42 : 3
3 ⑧ ili kwamba BWANA, Mungu wako, atuoneshe njia ambayo yatupasa tuiendee, na jambo litupasalo tulitende.

Yeremia 43 : 7
7 wakaingia nchi ya Misri; maana hawakuitii sauti ya BWANA; wakafika hadi Tapanesi.

1 Mambo ya Nyakati 3 : 15
15 Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.

1 Mambo ya Nyakati 3 : 24
24 Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 10
10 ⑮ na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)

1 Mambo ya Nyakati 12 : 4
4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;

1 Mambo ya Nyakati 12 : 12
12 Yohana wa nane, Elzabadi wa tisa;

2 Mambo ya Nyakati 28 : 12
12 Ndipo wakaondoka juu ya hao waliotoka vitani baadhi ya wakuu wa wana wa Efraimu, Azaria, mwana wa Yohanani, na Berekia mwana wa Meshilemothi, na Yehizkia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai,

Ezra 8 : 12
12 Na wa wana wa Azgadi, Yohana, mwana wa Hakatani; na pamoja naye wanaume mia moja na kumi.

Ezra 10 : 6
6 ⑩ Kisha Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu, akaingia katika chumba cha Yehohanani, mwana wa Eliashibu; hata, alipofika huko, hakula mkate, wala hakunywa maji; kwa maana alilia kwa sababu ya kosa lile la watu wa uhamisho.

Nehemia 12 : 23
23 ⑬ Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu hadi siku za Yohana mwana wa Eliashibu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *