Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yehohanani
1 Mambo ya Nyakati 26 : 3
3 Elamu wa tano, Yohana wa sita, Elioenai wa saba.
2 Mambo ya Nyakati 17 : 15
15 na wa pili wake Yehohanani kamanda, na pamoja naye elfu mia mbili na themanini;
2 Mambo ya Nyakati 23 : 1
1 Katika mwaka wa saba Yehoyada alijasiri, akawatwaa makamanda wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao.
Ezra 10 : 28
28 Na wa wazawa wa Bebai; Yehohanani, na Hanania, na Zakai, na Athlai.
Nehemia 12 : 13
13 wa Ezra, Meshulamu; wa Amaria, Yehohanani;
Nehemia 12 : 42
42 na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, akiwa Yezrahia msimamizi wao.
Leave a Reply