Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yehoahazi
2 Wafalme 10 : 35
35 Yehu akalala na babaze; wakamzika katika Samaria. Na Yehoahazi mwanawe akatawala mahali pake.
2 Wafalme 13 : 9
9 Yehoahazi akalala na babaze; wakamzika katika Samaria. Na Yehoashi[6] mwanawe akatawala mahali pake.
2 Wafalme 23 : 31
31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala; akatawala miezi mitatu katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali binti Yeremia wa Libna.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 15
15 Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 1
1 Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtawaza awe mfalme katika Yerusalemu mahali pa babaye.
Yeremia 22 : 11
11 Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za Shalumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; aliyemiliki badala ya Yosia, baba yake, yeye aliyetoka mahali hapa; Hatarudi huku tena;
2 Wafalme 23 : 32
32 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake.
2 Wafalme 23 : 35
35 Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao Neko.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 4
4 Mfalme wa Misri akamtawaza Eliakimu nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Neko akamtwaa Yehoahazi nduguye, akamchukua mpaka Misri.
Yeremia 22 : 12
12 bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.
Leave a Reply