Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wivu
Ayubu 5 : 3
3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara niliyalaani maskani yake.
Zaburi 37 : 1
1 Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.
Zaburi 37 : 7
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Mithali 24 : 19
19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya;
Zaburi 49 : 16
16 Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapoongezeka.
Zaburi 73 : 3
3 Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.
Zaburi 73 : 20
20 Ee Bwana, wamekuwa kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao.
Zaburi 112 : 10
10 ⑳ Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Mithali 3 : 31
31 Usimhusudu mtu mwenye ujeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
Mithali 14 : 30
30 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.
Mithali 23 : 17
17 Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa;
Mithali 24 : 1
1 Usiwawaonee wivu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao;
Mithali 27 : 4
4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Mhubiri 4 : 4
4 Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Wimbo ulio Bora 8 : 6
6 Nitie kama mhuri moyoni mwako, Kama mhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.
Isaya 26 : 11
11 BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
Ezekieli 35 : 11
11 ⑪ Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitatenda kwa kadiri ya hasira yako, na kwa kadiri ya wivu wako, ulioudhihirisha kwa kuwachukia; nami nitajidhihirisha kwao, nitakapokuhukumu wewe.
Warumi 1 : 29
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
Warumi 13 : 13
13 ⑧ Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
1 Wakorintho 3 : 3
3 ⑭ kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?
1 Wakorintho 13 : 4
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
2 Wakorintho 12 : 20
20 Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia;
Wagalatia 5 : 21
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wagalatia 5 : 26
26 ⑲ Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
1 Timotheo 6 : 5
5 na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Tito 3 : 3
3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
Yakobo 3 : 14
14 ⑱ Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
Yakobo 3 : 16
16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
Leave a Reply