Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wimbo
Mathayo 26 : 30
30 ⑥ Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda katika mlima wa Mizeituni.
Marko 14 : 26
26 ④ Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda katika mlima wa Mizeituni.⑤
Ufunuo 15 : 4
4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Zaburi 33 : 3
3 Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
Waefeso 5 : 19
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
Ufunuo 5 : 10
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Ufunuo 14 : 5
5 ⑲ Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.
Leave a Reply