Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wema
Warumi 8 : 28
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Zaburi 31 : 19
19 Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!
Zaburi 23 : 6
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 145 : 15 – 19
15 Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote.
18 ⑬ BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 ⑭ Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.
Wagalatia 5 : 22 – 23
22 ⑮ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 ⑯ upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Warumi 12 : 9
9 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema.
Yakobo 3 : 13
13 ⑰ Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Yohana 3 : 16 – 17
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Wagalatia 5 : 22
22 ⑮ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
Mika 6 : 8
8 Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
Yakobo 1 : 17
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Zaburi 27 : 13
13 ① Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.
Zaburi 25 : 7
7 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
Wagalatia 6 : 10
10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Zaburi 65 : 4
4 ① Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako.
Zaburi 34 : 8
8 ⑤ Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia.
Mathayo 12 : 35
35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
Tito 3 : 8 – 10
8 Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu.
9 ④ Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu.
10 ⑤ Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye;
2 Timotheo 3 : 16
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Mathayo 5 : 28 – 29
28 ⑯ lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 ⑰ Jicho lako la kulia likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote utupwe katika Jehanamu.
Leave a Reply