Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wazee
1 Timotheo 5 : 1 – 2
1 Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na wanaume vijana kama ndugu;
2 wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.
Mambo ya Walawi 19 : 32
32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.
Mithali 23 : 22
22 Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
Kutoka 20 : 12
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Isaya 40 : 28 – 31
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Mithali 20 : 29
29 Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
Leave a Reply