Biblia inasema nini kuhusu Watafutaji – Mistari yote ya Biblia kuhusu Watafutaji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Watafutaji

Mwanzo 49 : 18
18 Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.

Kumbukumbu la Torati 4 : 29
29 Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.

1 Mambo ya Nyakati 16 : 11
11 Mtafuteni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.

1 Mambo ya Nyakati 22 : 19
19 ⑲ Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.

1 Mambo ya Nyakati 28 : 9
9 ⑦ Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

2 Mambo ya Nyakati 11 : 16
16 Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.

2 Mambo ya Nyakati 15 : 2
2 naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.

2 Mambo ya Nyakati 15 : 13
13 na ya kwamba yeyote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, awe ni mwanamume au mwanamke.

2 Mambo ya Nyakati 26 : 5
5 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta BWANA, Mungu alimfanikisha.

2 Mambo ya Nyakati 30 : 19
19 aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, BWANA, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu.

2 Mambo ya Nyakati 31 : 21
21 ⑧ Na katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu wake, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa.

Ezra 8 : 22
22 Maana niliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni juu ya wote wamkataao.

Ayubu 5 : 8
8 ⑧ Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu kesi yangu;

Ayubu 8 : 6
6 Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

Zaburi 9 : 10
10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

Zaburi 14 : 2
2 Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.

Zaburi 17 : 2
2 Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili.

Zaburi 22 : 26
26 ⑰ Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele.

Zaburi 24 : 6
6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

Zaburi 25 : 5
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.

Zaburi 25 : 15
15 Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

Zaburi 27 : 4
4 Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.

Zaburi 27 : 8
8 Uliposema, “Nitafuteni uso wangu,” Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.

Zaburi 27 : 14
14 ② Umtumainie BWANA, uwe imara, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Zaburi 33 : 20
20 Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.

Zaburi 34 : 4
4 ② Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.

Zaburi 34 : 10
10 Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.

Zaburi 40 : 4
4 ⑭ Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *