Biblia inasema nini kuhusu wasumbufu – Mistari yote ya Biblia kuhusu wasumbufu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wasumbufu

Mithali 6 : 16 – 19
16 Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 ⑤ Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 ⑥ Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 ⑦ Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Warumi 12 : 18
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.

Mithali 20 : 3
3 ④ Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.

Warumi 16 : 17
17 ⑩ Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.

1 Petro 2 : 1 – 25
1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3 ① ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4 ② Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 ③ Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
6 ④ Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 ⑤ Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 ⑥ Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
9 ⑦ Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ⑧ ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
11 ⑩ Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 ⑪ Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
13 ⑫ Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme kama mwenye cheo kikubwa;
14 au iwe ni watawala, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.
15 ⑬ Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;
16 ⑭ kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.
17 ⑮ Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
18 ⑯ Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wale walio wema na wenye upole tu, bali pia wale walio wakali.
19 Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo pasipo haki.
20 ⑰ Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
21 ⑱ Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
22 ⑲ Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuwapo kinywani mwake.
23 ⑳ Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

Mathayo 5 : 44
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

Mathayo 5 : 9
9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Mithali 24 : 1 – 34
1 Usiwawaonee wivu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao;
2 Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara.
3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika,
4 Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
5 Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;
6 Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
7 Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni.
8 Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu;
9 Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.
11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.
12 Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
13 Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.
14 Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.
15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
16 ① Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
17 Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake.
19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya;
20 ② Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika.
21 ③ Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu;
22 Maana msiba wao utatokea kwa ghafla; Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao.
23 ④ Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema.
24 ⑤ Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia.
25 Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
26 Aibusu midomo atoaye jawabu la haki.
27 Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.
28 ⑥ Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako.
29 ⑦ Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.
30 Nilipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 ⑧ Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Niliona, nikapata mafundisho.
33 ⑩ Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Waefeso 6 : 12
12 ⑧ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *