Biblia inasema nini kuhusu warumi – Mistari yote ya Biblia kuhusu warumi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia warumi

Warumi 15 : 25 – 27
25 Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumia watakatifu;
26 maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kutoa mchango kwa ajili ya watakatifu walio maskini huko Yerusalemu.
27 ① Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumia kwa mambo yao ya mwili.

Warumi 15 : 15 – 16
15 Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,
16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.

Warumi 13 : 14
14 ⑩ Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.

Warumi 16 : 1 – 6
1 Namkabidhi kwenu Fibi, dada yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea;
2 ili mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lolote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
3 ④ Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu;
4 waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao.
5 ⑤ Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
6 Nisalimieni Mariamu, aliyejishughulisha sana kwa ajili yenu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *