Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wapelethi
1 Wafalme 1 : 38
38 Basi wakashuka Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Wakerethi, na Wapelethi, wakampandisha Sulemani juu ya nyumbu wa mfalme Daudi, wakampeleka mpaka Gihoni.
2 Samweli 8 : 18
18 ⑧ na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.
2 Samweli 20 : 7
7 ⑯ Ndipo wakatoka nyuma yake watu wa Yoabu, na Wakerethi na Wapelethi, na mashujaa wote; wakatoka Yerusalemu, ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri.
2 Samweli 20 : 23
23 Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi;
1 Mambo ya Nyakati 18 : 17
17 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa mofisa wakuu wa mfalme.
2 Samweli 15 : 18
18 ⑱ Watumishi wake wote wakapita karibu naye; na Wakerethi wote, na Wapelethi wote, na Wagiti wote, watu mia sita walioandamana naye kutoka Gathi, wakapita mbele ya mfalme.
Leave a Reply