Biblia inasema nini kuhusu Waovu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Waovu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Waovu

Isaya 14 : 19
19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.

Malaki 4 : 3
3 ⑪ Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.

Mathayo 13 : 48
48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.

Zaburi 49 : 12
12 Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.

2 Petro 2 : 12
12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

Sefania 1 : 17
17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.

Mathayo 15 : 14
14 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Yeremia 6 : 28
28 ⑦ Ni waasi kupita kiasi wote pia, waendao huku na huko wakisingizia, ni shaba na chuma hao, hutenda dhuluma wote pia.

Ezekieli 22 : 18
18 ⑦ Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa taka za fedha kwangu; wote wamekuwa shaba, na bati, na chuma, na risasi, katika tanuri; wamekuwa taka za fedha.

Isaya 55 : 13
13 Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

Ezekieli 2 : 6
6 Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.

Zaburi 22 : 12
12 Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga;

Isaya 14 : 19
19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.

Ayubu 21 : 18
18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba?

Zaburi 1 : 4
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

Mathayo 3 : 12
12 ⑫ Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

2 Wafalme 19 : 26
26 Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *