Biblia inasema nini kuhusu Wanaorudi nyuma – Mistari yote ya Biblia kuhusu Wanaorudi nyuma

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wanaorudi nyuma

Mambo ya Walawi 26 : 42
42 ⑭ ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.

Kumbukumbu la Torati 4 : 9
9 ⑩ Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;

Kumbukumbu la Torati 8 : 14
14 ⑯ basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;

Kumbukumbu la Torati 28 : 68
68 ⑰ BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.

1 Wafalme 9 : 9
9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu BWANA ameleta mabaya haya yote juu yao.

Kumbukumbu la Torati 29 : 28
28 BWANA akawang’oa katika nchi yao kwa hasira, na ghadhabu, na makamio makuu, akawatupa waende nchi nyingine, kama hivi leo.

Kumbukumbu la Torati 32 : 30
30 Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?

Yoshua 24 : 27
27 Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.

2 Mambo ya Nyakati 15 : 4
4 lakini walipomgeukia BWANA, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao.

Ezra 8 : 22
22 Maana niliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni juu ya wote wamkataao.

Ayubu 34 : 27
27 Kwa sababu walikengeuka, wasimfuate yeye, Wasikubali kuzishika njia zake hata moja;

Zaburi 44 : 21
21 ⑤ Je! Mungu hangegundua jambo hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo.

Zaburi 73 : 27
27 Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.

Zaburi 85 : 8
8 ⑲ Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA, Maana atawaambia watu wake amani, Naam, na watauwa wake pia, Bali wasiurudie upumbavu tena.

Zaburi 125 : 5
5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.

Mithali 2 : 17
17 Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake.

Mithali 14 : 14
14 Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.

Mithali 24 : 16
16 ① Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.

Mithali 26 : 11
11 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.

Yeremia 17 : 13
13 Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.

Ezekieli 3 : 20
20 ⑮ Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

Ezekieli 18 : 24
24 ⑭ Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.

Ezekieli 18 : 26
26 Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.

Ezekieli 23 : 35
35 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umenisahau, na kunitupa nyuma yako, basi kwa hiyo, uchukue uasherati wako na uzinzi wako.

Ezekieli 33 : 13
13 ⑱ Japo ninapomwambia mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akitenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.

Ezekieli 33 : 18
18 Mwenye haki ageukapo, na kuiacha haki yake, na kutenda maovu, atakufa katika maovu hayo.

Hosea 11 : 8
8 ⑧ Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *