Biblia inasema nini kuhusu Wahivi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Wahivi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wahivi

Mwanzo 10 : 17
17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,

1 Mambo ya Nyakati 1 : 15
15 na Mhivi, na Mwarki, na Msini;

Mwanzo 34 : 2
2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.

Yoshua 9 : 7
7 ⑪ Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mnakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi?

Yoshua 11 : 19
19 ⑮ Haukuwapo mji hata mmoja uliofanya amani na wana wa Israeli, isipokuwa ni wale Wahivi waliokaa Gibeoni; wakaitwaa yote kwa vita.

Mwanzo 26 : 34
34 ⑬ Esau alipokuwa mwenye miaka arubaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti.

Mwanzo 36 : 2
2 Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi;

Yoshua 11 : 3
3 ⑧ na kwa Mkanaani upande wa mashariki, na upande wa magharibi, na kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi na Myebusi katika nchi ya vilima, na kwa Mhivi pale chini ya Hermoni katika nchi ya Mispa.

Waamuzi 3 : 3
3 ⑱ aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.

2 Samweli 24 : 7
7 wakaja ngomeni kwa Tiro, na kwa miji yote ya Wahivi, na ya Wakanaani; tena wakaenda katika Negebu ya Yuda huko Beer-sheba.

Kutoka 23 : 23
23 ④ Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawatupilia mbali.

Kutoka 23 : 28
28 ⑩ Nami nitapeleka mavu[26] mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.

Kumbukumbu la Torati 20 : 17
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako;

Waamuzi 3 : 5
5 ⑲ Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi;

Yoshua 9 : 1
1 ⑤ Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo;

Yoshua 12 : 8
8 katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika materemko, na katika nyika, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

Yoshua 24 : 11
11 ⑩ Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu.

1 Wafalme 9 : 21
21 watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.

2 Mambo ya Nyakati 8 : 8
8 wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *