Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wafungwa
Waraka kwa Waebrania 13 : 3
3 Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili.
Mathayo 25 : 35 – 46
35 kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha; nilikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nilikuwa uchi, mkanivika nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nilikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona ukiwa na njaa, tukakulisha, au ukiwa na kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona ukiwa mgeni, tukakukaribisha, au ukiwa uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona ukiwa mgonjwa, au ukiwa kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nilikuwa na njaa, msinipe chakula; nilikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nilikuwa mgeni, msinikaribishe; nilikuwa uchi, msinivike; nilikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe ukiwa na njaa, au ukiwa na kiu, au ukiwa mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Zaburi 69 : 33
33 Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.
Zaburi 102 : 20
20 Ili akisikie kilio cha kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
Isaya 61 : 1
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Zaburi 146 : 7
7 Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; BWANA hufungua waliofungwa;
Mwanzo 39 : 20 – 23
20 ⑤ Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani.
21 ⑥ Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
22 ⑦ Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliokuwemo gerezani; na yote yaliyofanywa humo, yeye ndiye aliyeyafanya.
23 ⑧ Wala mkuu wa gereza hakufuatilia kazi liliyokuwa mikononi mwa Yusufu; kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya.
Isaya 42 : 7
7 ⑰ kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Zaburi 79 : 11
11 Kuugua kwake aliyefungwa Na kuingie mbele zako. Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako Uwahifadhi waliohukumiwa kufa.
Luka 4 : 18
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
Waefeso 4 : 22 – 24
22 ⑧ mvue mwenendo wenu wa kwanza, utu wa zamani unaoharibika, kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
23 ⑩ na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
24 ⑪ na mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kutoka 23 : 7
7 Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.
Leave a Reply