Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wafu
1 Wafalme 17 : 23
23 Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka ghorofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.
2 Wafalme 4 : 37
37 Ndipo akaingia, akamwangukia miguu akainama mpaka nchi; kisha akamchukua mwanawe, akatoka.
2 Wafalme 13 : 21
21 ③ Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Luka 7 : 15
15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.
Luka 8 : 55
55 Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.
Yohana 11 : 44
44 Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Matendo 9 : 40
40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
Matendo 20 : 12
12 Wakamleta yule kijana, akiwa mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.
Waraka kwa Waebrania 11 : 35
35 ⑩ Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;
Matendo 9 : 37
37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; wakati walipokwisha kumwosha, wakamweka ghorofani.
Mathayo 26 : 12
12 Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.
2 Mambo ya Nyakati 16 : 14
14 ② Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
2 Mambo ya Nyakati 21 : 19
19 Ikawa baada ya siku, kufika mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatokea kwa sababu ya ugonjwa wake, akafa akiwa kwenye maumivu makali. Wala watu wake hawakuwasha moto kuombolezea kifo chake kama walivyowafanyia baba zake.
Yeremia 34 : 5
5 utakufa katika amani; na kama walivyofukizia baba zako, wafalme wa zamani waliokutangulia, ndivyo watakavyokufukizia; na kukulilia wakisema, Aa, BWANA! Kwa maana mimi nimelinena neno hili, asema BWANA.
Leave a Reply