Biblia inasema nini kuhusu Vumbi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Vumbi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Vumbi

Mwanzo 2 : 7
7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.

Mwanzo 3 : 19
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Mwanzo 3 : 23
23 kwa hiyo BWANA Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.

Mhubiri 3 : 20
20 ⑳ Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

2 Samweli 16 : 13
13 Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; Shimei naye akaaendelea juu ya ubavu wa kile kilima, kwa kumkabili, huku akiendelea, akilaani, akimtupia mawe, na kurusha mavumbi.

Mathayo 10 : 14
14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

Matendo 13 : 51
51 Nao wakawakung’utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.

Yoshua 7 : 6
6 ⑯ Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.

1 Samweli 4 : 12
12 Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle vitani akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake.

2 Samweli 1 : 2
2 hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.

2 Samweli 15 : 30
30 Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akapanda huku akilia; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.

Ayubu 2 : 12
12 Basi walipoinua macho yao, wakiwa bado kwa mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho lake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.

Ayubu 42 : 6
6 Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *