Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Viungo
Kutoka 25 : 6
6 na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;
Kutoka 35 : 8
8 na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri;
2 Wafalme 20 : 13
13 ⑫ Hezekia akawasikiliza, akawaonesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.
1 Mambo ya Nyakati 9 : 29
29 Na baadhi yao waliwajibika kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; pamoja na unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.
Mwanzo 37 : 25
25 ⑧ Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.
Mwanzo 43 : 11
11 Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
1 Wafalme 10 : 2
2 Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni.
1 Wafalme 10 : 10
10 Basi akampa mfalme talanta za dhahabu mia moja na ishirini, na manukato mengi, mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja tena wingi wa manukato, kama hayo malkia wa Sheba aliyompa mfalme Sulemani.
Ezekieli 27 : 22
22 ⑥ Wachuuzi wa Sheba, na Raama, ndio waliokuwa wachuuzi wako; badala ya vitu vyako walitoa manukato yaliyo mazuri, na kila aina ya vito vya thamani, na dhahabu.
2 Mambo ya Nyakati 16 : 14
14 ② Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Marko 16 : 1
1 Na sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.
Luka 23 : 56
56 ⑭ Wakarudi, wakatayarisha manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.
Luka 24 : 1
1 ⑮ Siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Yohana 19 : 40
40 Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Leave a Reply