Biblia inasema nini kuhusu vito – Mistari yote ya Biblia kuhusu vito

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia vito

Ufunuo 21 : 11
11 ⑩ ukiwa na utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;

Malaki 3 : 17
17 Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.

Mithali 20 : 15
15 Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.

Ezekieli 16 : 11 – 13
11 Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.
12 Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.
13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.

1 Timotheo 2 : 9
9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

Mithali 31 : 10
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.

Ufunuo 4 : 1 – 11
1 Baada ya hayo niliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
2 Na mara nilikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;
3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.
4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti niliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wameikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji la dhahabu.
5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
9 Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,
10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.

Zaburi 103 : 2 – 4
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 ⑤ Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema,

Kutoka 39 : 1 – 43
1 ⑤ Na zile nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyatengeneza hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
2 ⑥ Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa.
3 Nao wakaifua hiyo dhahabu hata ikawa mabamba membamba sana, kisha wakaikata iwe nyuzi, ili wapate kuifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyuzi nyekundu na za kitani nzuri, kazi ya fundi stadi sana.
4 Nao wakafanya na vipande vya mabegani kwa ajili yake, vilivyoungwa pamoja; viliungwa pamoja kwa ncha zake mbili.
5 ⑦ Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
6 ⑧ Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake mhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli.
7 ⑩ Naye akavitia katika vile vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
8 ⑪ Naye akafanya kile kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi, kama hiyo kazi ya naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa.
9 Kilikuwa mraba; wakakifanya kile kifuko cha kifuani kwa kukikunja; urefu wake ulikuwa shibiri, na upana wake ulikuwa shibiri, tena kilikuwa ni cha kukunjwa.
10 ⑫ Nao wakatia safu nne za vito ndani yake, safu moja ilikuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, vilikuwa ni safu ya kwanza.
11 ⑬ Na safu ya pili ilikuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi.
12 Na safu ya tatu ilikuwa ni hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto.
13 ⑭ Na safu ya nne ilikuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi: vito hivyo vilikuwa vimetiwa katika vijalizo vya dhahabu, kila kimoja mahali pake.
14 Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora mihuri, kila moja kwa jina lake, kwa yale makabila kumi na mawili.
15 Nao wakafanya katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa ya dhahabu safi.
16 Nao wakafanya vijalizo viwili vya dhahabu, na pete mbili za dhahabu; nao wakazitia hizo pete mbili katika ncha mbili za hicho kifuko.
17 Nao wakaitia hiyo mikufu miwili iliyosokotwa katika hizo pete mbili zilizokuwa katika ncha mbili za hicho kifuko.
18 Na ncha hizo mbili nyingine, za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa, wakazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera, upande wa mbele.
19 Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani.
20 Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
21 Nao wakakikaza kile kifuko kwa pete zake kwenye naivera kwa ukanda wa rangi ya samawati, ili kikae pale juu ya mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, na ya kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
22 ⑮ Naye akafanya hilo joho la naivera ya kazi ya kusuka, rangi ya samawati yote;
23 na hilo tundu lililokuwa katikati yake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, na utepe wake kulizunguka hilo tundu, ili lisipasuke.
24 Nao wakatia katika upindo wa joho makomamanga ya nyuzi za rangi ya samawati, na rangi ya zambarau, na rangi nyekundu, na kitani iliyosokotwa.
25 ⑯ Nao wakafanya njuga za dhahabu safi, na kuzitia hizo njuga kati ya hayo makomamanga pande zote, kati ya hayo makomamanga;
26 njuga na komamanga, njuga na komamanga katika pindo za joho kuizunguka pande zote, ili kutumika kwa hiyo; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
27 ⑰ Nao wakafanya hizo kanzu za nguo ya kitani nzuri ya kufumwa, kwa Haruni, na kwa wanawe
28 ⑱ na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa,
29 na huo mshipi wa nguo nzuri ya kitani iliyosokotwa, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, kazi ya fundi mwenye kutia taraza; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
30 ⑲ Nao wakafanya hilo bamba la hilo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa mhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.
31 Nao wakatia ukanda wa rangi ya samawati ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
32 ⑳ Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.
33 Nao wakamletea Musa hiyo maskani; yaani Hema, na vyombo vyake vyote, vifungo vyake, na mbao zake, na mataruma yake, na nguzo zake, na vitako yake;
34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo, na pazia la sitara;
35 na sanduku la ushuhuda, na miti yake, na kiti cha rehema;
36 na meza, na vyombo vyake vyote, na mikate ya wonyesho;
37 na kinara cha taa safi, na taa zake, hizo taa za kuwekwa mahali pake, na vyombo vyake vyote, na mafuta ya taa,
38 na madhabahu ya dhahabu, na mafuta ya kutiwa, na uvumba mzuri, na pazia kwa mlango wa hema;
39 na madhabahu ya shaba, na wavu wake wa shaba, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake;
40 na ukuta wa nguo wa ua, na nguzo zake na vitako vyake, na pazia la lango la ua, na kamba zake, na vigingi vyake, na vyombo vyote vya kutumiwa katika utumishi wa maskani, kwa hiyo hema ya kukutania,
41 na mavazi ya kazi nzuri kwa utumishi katika mahali patakatifu, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.
42 Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli.
43 Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *