Biblia inasema nini kuhusu Vita – Mistari yote ya Biblia kuhusu Vita

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Vita

Waamuzi 7 : 20
20 Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa BWANA na wa Gideoni.

1 Samweli 17 : 20
20 Daudi akaondoka asubuhi na mapema, akawaacha kondoo pamoja na mchungaji, akavitwaa vitu vile, akaenda, kama Yese alivyomwamuru; akafika penye magari, wakati lile jeshi walipokuwa wakitoka kwenda kupigana, wakipiga kelele za vita.

2 Mambo ya Nyakati 13 : 12
12 ⑮ Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye parapanda, ili wapige sauti ya kuanza vita juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na BWANA, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.

2 Mambo ya Nyakati 14 : 11
11 Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *