Biblia inasema nini kuhusu viapo – Mistari yote ya Biblia kuhusu viapo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia viapo

Mathayo 5 : 33 – 37
33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndipo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Yakobo 5 : 12
12 Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali “ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, msije mkaanguka katika hukumu.

Hesabu 30 : 2
2 Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.

Waraka kwa Waebrania 6 : 13
13 Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,

Waraka kwa Waebrania 6 : 17
17 Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;

Zaburi 15 : 4
4 Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.

Matendo 23 : 12 – 14
12 Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo.
13 Na hao walioapiana hivyo walikuwa zaidi ya watu arubaini.
14 Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo.

Mathayo 23 : 18 – 22
18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga kwa kiapo.
19 ⑭ Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka?
20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake.
22 ⑮ Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.

Waraka kwa Waebrania 7 : 28
28 ⑭ Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.

Waraka kwa Waebrania 3 : 11
11 ⑤ Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.

Waraka kwa Waebrania 3 : 18
18 ⑫ Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi?

Waraka kwa Waebrania 7 : 21
21 ⑧ (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;)

Yohana 6 : 67 – 71
67 Basi Yesu akawaambia wale Kumi na Wawili, Je! Ninyi nanyi mnataka kuondoka?
68 ⑭ Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
69 ⑮ Nasi tumeamini, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.
70 Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Kumi na Wawili, na mmoja wenu ni shetani?
71 Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Kumi na Wawili.

Kumbukumbu la Torati 23 : 21 – 23
21 Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.
22 Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.
23 Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.

Luka 1 : 73
73 ⑪ Kiapo alichomwapia Abrahamu, baba yetu,

Mathayo 14 : 3 – 12
3 ⑱ Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye.
4 ⑲ Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye.
5 ⑳ Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii.
6 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
7 Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lolote atakaloliomba.
8 Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.
9 Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi karamuni pamoja naye, akaamuru apewe;
10 akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.
11 Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule msichana; akakileta kwa mamaye.
12 Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.

Waraka kwa Waebrania 4 : 3
3 ⑭ Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia pumzikoni mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Waraka kwa Waebrania 6 : 16
16 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao mwisho wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.

Waraka kwa Waebrania 6 : 14
14 akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.

Wagalatia 1 : 20
20 Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *