Biblia inasema nini kuhusu Uzuri โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu Uzuri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzuri

Zaburi 39 : 11
11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.

Mithali 6 : 25
25 โ‘ช Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.

Mithali 31 : 30
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.

Isaya 3 : 24
24 Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.

Ezekieli 16 : 14
14 Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU.

Ezekieli 28 : 17
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

Zaburi 39 : 11
11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.

Zaburi 49 : 14
14 Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.

Mwanzo 12 : 11
11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso;

Mwanzo 24 : 16
16 Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.

Mwanzo 29 : 17
17 Naye Lea macho yake yalikuwa malegevu,[12] lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri wa uso.

Mwanzo 39 : 6
6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu chochote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.

Kutoka 2 : 2
2 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.

Waraka kwa Waebrania 11 : 23
23 Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme.

1 Samweli 16 : 12
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.

1 Samweli 16 : 18
18 Ndipo mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mtoto mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye BWANA yuko pamoja naye.

2 Samweli 11 : 2
2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

2 Samweli 13 : 1
1 โ‘ซ Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na dada yake mzuri, aliyeitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.

2 Samweli 14 : 25
25 Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake.

1 Wafalme 1 : 4
4 Naye msichana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; lakini mfalme hakumjua.

Esta 1 : 11
11 wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, akiwa amevaa taji la kifalme; ili kuwaonesha watu na wakuu uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *