Biblia inasema nini kuhusu Uziwi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uziwi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uziwi

Mambo ya Walawi 19 : 14
14 ⑱ Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.

Kutoka 4 : 11
11 BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?

Mathayo 11 : 5
5 ⑳ vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.

Marko 7 : 32
32 Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.

Marko 9 : 25
25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.

Isaya 6 : 10
10 Zifanye akili za watu hawa zipumbae, na uyatie uzito masikio yao, na uyafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.

Isaya 29 : 18
18 Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.

Isaya 35 : 5
5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

Ezekieli 12 : 2
2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.

Mathayo 13 : 15
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Yohana 12 : 40
40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *