Biblia inasema nini kuhusu Uzieli – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uzieli

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzieli

Kutoka 6 : 18
18 Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.

Kutoka 6 : 22
22 Na wana wa Uzieli; ni Mishaeli, na Elisafani, na Sithri.

Mambo ya Walawi 10 : 4
4 Musa akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjombaye Haruni, na kuwaambia, Njoni karibu, mwachukue hawa ndugu zenu, mkawaondoe hapa mbele ya maskani, mwende nao nje ya kambi.

1 Mambo ya Nyakati 4 : 42
42 Na baadhi yao, wana wa Simeoni wapatao watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.

1 Mambo ya Nyakati 7 : 7
7 Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne.

1 Mambo ya Nyakati 25 : 4
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

2 Mambo ya Nyakati 29 : 14
14 na wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana wa Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.

Nehemia 3 : 8
8 ④ Na baada yao akajenga Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *