Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzee
Mwanzo 15 : 15
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
Mwanzo 47 : 9
9 ③ Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao.
Kumbukumbu la Torati 34 : 7
7 Musa alikuwa mtu wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.
2 Samweli 19 : 37
37 ⑥ Niache nirudi basi, mimi mtumishi wako, ili nife katika mji wangu mwenyewe, karibu na kaburi la baba yangu na la mama yangu. Lakini tazama, mtumishi wako Kimhamu; na avuke yeye pamoja na bwana wangu mfalme; nawe ukamtendee yeye yaliyo mema machoni pako.
1 Mambo ya Nyakati 29 : 28
28 Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.
Ayubu 5 : 26
26 Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.
Ayubu 11 : 17
17 Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Giza lake litakuwa kama alfajiri.
Ayubu 42 : 17
17 Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana mwenye kujawa na siku.
Ayubu 12 : 12
12 Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
Ayubu 32 : 9
9 Sio wakuu walio wenye hekima, Wala sio wazee watambuao haki.
Zaburi 71 : 9
9 Usinitupe wakati wa uzee, Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
Zaburi 71 : 18
18 Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Zaburi 90 : 10
10 Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Zaburi 92 : 14
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
Zaburi 148 : 13
13 Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
Mithali 16 : 31
31 Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.
Mhubiri 6 : 3
3 Mtu akizaa watoto mia moja, akaishi miaka mingi, hata siku za maisha yake zikiwa nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;
Mhubiri 6 : 6
6 naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja?
Mhubiri 12 : 7
7 ⑤ Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Isaya 46 : 4
4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Luka 2 : 37
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
Tito 2 : 3
3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema;
Leave a Reply