Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uzee
Mithali 16 : 31
31 Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.
Ayubu 12 : 12
12 Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
Isaya 46 : 4
4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Zaburi 71 : 18
18 Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Tito 2 : 2
2 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika subira.
Zaburi 92 : 14
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
Zaburi 71 : 9
9 Usinitupe wakati wa uzee, Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
Mambo ya Walawi 19 : 32
32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.
Zaburi 90 : 10
10 Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Mithali 20 : 29
29 Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
Ayubu 5 : 26
26 Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.
2 Wakorintho 4 : 16
16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Mwanzo 6 : 3
3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.
Ayubu 11 : 17
17 Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Giza lake litakuwa kama alfajiri.
Zaburi 148 : 12
12 Vijana wa kiume, na wanawali, Wazee, na watoto;
Ruthu 4 : 15
15 Naye atakurejeshea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
Kumbukumbu la Torati 33 : 25
25 Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
Leave a Reply