Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uwezo
2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Mambo ya Walawi 18 : 1 – 30
1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao.
4 Mtayatii maagizo yangu, na mtazishika amri zangu, ili kuzifuata; mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
5 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
6 Mtu yeyote miongoni mwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA.
7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
9 Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue.
10 Utupu wa binti ya mwanao wa kiume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ni utupu wako mwenyewe.
11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake.
12 Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu.
13 Usifunue utupu wa dada ya mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako wa karibu.
14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi yako.
15 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.
16 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.
17 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanaye wa kiume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.
18 ① Wala usitwae[7] mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai.
19 ② Usimwendee mwanamke kufunua utupu wake atakapokuwa najisi kwa ajili ya hedhi.
20 ③ Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.
21 ④ Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki[8] na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.
22 ⑤ Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
23 ⑥ Wala usilale na mnyama yeyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni upotovu.
24 ⑦ Msijitie unajisi katika hata mojawapo ya mambo hayo; kwa maana hayo mataifa nitakayoyatoa mbele zenu yamekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
25 ⑧ nayo nchi ikawa najisi; na nikaipatiliza kwa ajili ya uovu wake, kisha ikawatema wakazi wake.
26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na maagizo yangu, wala msifanye mojawapo ya machukizo hayo; yeye aliye mzaliwa, wala mgeni aishiye kati yenu;
27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ili hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
29 Kwani mtu yeyote atakayefanya mojawapo ya machukizo hayo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.
30 Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Mithali 22 : 6
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Zaburi 1 : 1 – 1
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Leave a Reply