Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uvumilivu
1 Wakorintho 5 : 11
11 ⑤ Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
2 Yohana 1 : 10 – 11
10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
2 Timotheo 4 : 1 – 2
1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Kumbukumbu la Torati 13 : 6 – 10
6 Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
7 katika miungu ya mataifa yaliyo kandokando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;
8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;
9 mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote.
10 Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na BWANA, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Waefeso 4 : 2
2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;
Yohana 8 : 7
7 ⑩ Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Warumi 14 : 1 – 4
1 ⑪ Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, lakini msimhukumu mawazo yake.
2 ⑫ Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
3 ⑬ Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.
4 ⑭ Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Matendo 10 : 28
28 Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali kwa mtu aliye Myahudi ashirikiane na mtu wa taifa lingine wala kumtembelea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi.
Mathayo 7 : 12
12 ⑰ Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
1 Timotheo 6 : 3 – 5
3 Mtu awaye yote akitoa mafundisho mengine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
4 amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matusi, na shuku mbaya;
5 na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Mithali 16 : 24
24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
Zaburi 133 : 1
1 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
Kutoka 14 : 14
14 ⑦ BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Ufunuo 2 : 2
2 Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;
Waefeso 5 : 15
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
1 Wakorintho 6 : 1 – 4
1 Je! Mmoja wenu akiwa ana shtaka juu ya mwenzake athubutuje kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
2 ⑧ Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?
Leave a Reply