Biblia inasema nini kuhusu utumishi – Mistari yote ya Biblia kuhusu utumishi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia utumishi

Luka 22 : 27
27 ⑱ Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.

Wafilipi 2 : 7
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

Wafilipi 2 : 1 – 30
1 Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema,
2 ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.
3 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuko na namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
14 ① Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,
15 ② mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
16 ③ mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.
17 ④ Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18 ⑤ Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.
19 Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
20 ⑥ Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli.
21 ⑦ Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.
22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
23 Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata.
24 ⑧ Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibuni.
25 ⑩ Lakini niliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mfanyakazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
26 Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa mgonjwa.
27 Kwa maana alikuwa mgonjwa sana, karibu kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
28 Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu.
29 ⑪ Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.
30 Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akahatarisha roho yake ili kusudi aitimize huduma ambayo msingeweza kunitimizia.

Yohana 13 : 1 – 38
1 Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, huku akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye akiwa amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
2 Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;
3 Yesu, huku akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Akamfikia Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe waniosha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutaniosha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Nisipokuosha, huna shirika nami.
9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga mwili[3] hana haja ila ya kuosha miguu, maana yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
12 Basi alipokwisha kuwaosha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa hayo niliyowatendea?
13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, imewapasa ninyi pia kuoshana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyemtuma.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
18 Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
19 Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.
20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenituma.
21 Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.
22 Wanafunzi wakatazamana, huku wakiwa na mashaka ni nani amnenaye.
23 Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.
24 Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?
25 Basi yeye, huku akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?
26 Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti.
27 Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.
28 Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.
29 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
30 Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku.
31 Basi huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake.
32 Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.
33 Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
36 ① Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye. ②
37 Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako.
38 Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hadi wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.

Wakolosai 3 : 17
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.

Waefeso 5 : 21
21 Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

Mathayo 20 : 25 – 28
25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
26 ① Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
27 na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;
28 ② kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *