Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia utulivu
Zaburi 46 : 10
10 ⑰ Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Kutoka 14 : 14
14 ⑦ BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 14 : 13
13 ⑥ Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
Ruthu 2 : 12
12 BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.
Hesabu 9 : 8
8 Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakaloagiza juu yenu.
Leave a Reply