Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ustoa
Mathayo 3 : 4
4 ⑥ Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Mathayo 11 : 18
18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo.
Luka 7 : 33
33 ⑧ Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo.
Mathayo 10 : 39
39 ⑬ Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
Mathayo 16 : 24
24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Marko 8 : 35
35 ⑰ Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
Luka 9 : 26
26 ④ Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
Luka 14 : 27
27 ⑧ Mtu yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Mathayo 10 : 37
37 ⑪ Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Luka 14 : 26
26 ⑥ Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. ⑦
Warumi 7 : 24
24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
1 Wakorintho 9 : 27
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Leave a Reply