Biblia inasema nini kuhusu usonji – Mistari yote ya Biblia kuhusu usonji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia usonji

Yohana 9 : 1 – 3
1 ③ Na alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.
2 ④ Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
3 ⑤ Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.

1 Wakorintho 12 : 18
18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

Isaya 54 : 13
13 ⑬ Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Zaburi 139 : 1 – 24
1 ⑰ Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.
2 ⑱ Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
4 ⑲ Maana hamna neno katika ulimini wangu Usilolijua kabisa, BWANA.
5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 ⑳ Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kulia utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17 Mawazo yako ni mazito sana kwangu; Ee Mungu; nayo ni makuu sana.
18 Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe.
19 Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;
20 Wale wanaokusema kwa ubaya, na kutenda maovu juu ya jina lako bure.
21 Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiudhike nao watu wanaokuasi?
22 Nawachukia kwa upepo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu.
23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Kutoka 4 : 11
11 BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?

Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mathayo 17 : 14 – 18
14 Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema,
15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini.
16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.
17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu.
18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule mvulana akapona tangu saa ile.

Yohana 3 : 17
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

1 Wakorintho 1 : 26 – 29
26 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.

Marko 9 : 17 – 29
17 Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;
18 na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.
19 Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.
20 Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu.
21 Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto.
22 Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia.
23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.
24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutoamini kwangu.
25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
26 Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.
27 Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.
28 Alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba.[5]

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *