Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uso
Mithali 25 : 23
23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
Ayubu 29 : 24
24 Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
Zaburi 4 : 6
6 Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema? BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.
Zaburi 21 : 6
6 Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.
Zaburi 44 : 3
3 Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.
Mithali 15 : 13
13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.
Mithali 27 : 17
17 Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Kumbukumbu la Torati 28 : 50
50 ④ taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
Danieli 8 : 23
23 Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosaji watakapotimia kilele cha uovu wao, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.
Mwanzo 4 : 5
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
Isaya 3 : 9
9 Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Zaburi 42 : 11
11 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Zaburi 43 : 5
5 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Maana nitamsifu tena, Aliye msaada wangu, Na Mungu wangu.
2 Wafalme 5 : 1
1 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Zaburi 10 : 4
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;
Mwanzo 31 : 2
2 ⑫ Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama hapo awali.
Mwanzo 31 : 5
5 ⑭ Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama hapo awali. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami.
1 Samweli 1 : 18
18 Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukuhuzunika tena.
Nehemia 2 : 3
3 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?
Mhubiri 7 : 3
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
Ezekieli 27 : 35
35 ⑭ Wote wakaao katika visiwa vile watakustaajabia, na wafalme wao wameogopa sana, wamefadhaika nyuso zao.
Danieli 1 : 15
15 Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
Danieli 1 : 6
6 Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria.
Kutoka 34 : 35
35 Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling’aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.
Leave a Reply