Biblia inasema nini kuhusu ushujaa – Mistari yote ya Biblia kuhusu ushujaa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ushujaa

2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

1 Wakorintho 16 : 13
13 ⑩ Kesheni, simameni imara katika imani, iweni na ujasiri, mkawe hodari.

1 Mambo ya Nyakati 28 : 20
20 ⑮ Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA.

Wafilipi 1 : 28
28 wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lolote; kwao hao ni ishara thabiti ya kuangamizwa, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.

Kumbukumbu la Torati 31 : 6
6 ⑦ Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.

Warumi 8 : 26 – 27
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Zaburi 29 : 1 – 11
1 ⑤ Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
2 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
3 Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.
4 Sauti ya BWANA ina nguvu; Sauti ya BWANA ina utukufu;
5 Sauti ya BWANA yaivunja mierezi; Naam, BWANA aivunjavunja mierezi ya Lebanoni;
6 ⑥ Airusharusha Lebanoni kama ndama wa ng’ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwananyati.
7 Sauti ya BWANA inatoa miale paa ya moto;
8 ⑦ Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa; BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.
9 Sauti ya BWANA yawazalisha ayala, Na kuiacha misitu wazi; Na ndani ya hekalu lake Wanasema, Utukufu!
10 ⑧ BWANA aketi juu ya Gharika; Naam, BWANA ameshika hatamu ya ufalme milele.
11 ⑩ BWANA na awape watu wake nguvu; BWANA na awabariki watu wake kwa amani.

Mathayo 28 : 20
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

2 Timotheo 4 : 22
22 Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi.

Ayubu 23 : 10
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

1 Wakorintho 2 : 3
3 Nami nilikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na kwa kutetemeka sana.

1 Petro 5 : 2 – 5
2 ⑬ lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
3 ⑭ Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi.
4 ⑮ Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtalipokea taji la utukufu, lile lisilokauka.
5 ⑯ Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

Yoshua 1 : 9
9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

1 Petro 1 : 2
2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

Mithali 1 : 7
7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Tito 3 : 10
10 ⑤ Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *