Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ushuhuda
1 Mambo ya Nyakati 16 : 9
9 Mwimbieni, mwimbieni nyimbo za kumsifu; Yatangazeni matendo yake yote ya ajabu.
Zaburi 9 : 11
11 Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni, Yatangazeni kwa watu matendo yake.
Zaburi 18 : 49
49 Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
Zaburi 26 : 7
7 Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.
Zaburi 119 : 27
27 Unifahamishe njia ya maagizo yako, Nami nitayatafakari maajabu yako.
Zaburi 119 : 172
172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, Maana maagizo yako yote ni ya haki.
Zaburi 145 : 12
12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Isaya 12 : 6
6 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Isaya 32 : 4
4 Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa.
Isaya 43 : 10
10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine.
Isaya 44 : 8
8 ② Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuambia haya zamani na kuyatangaza? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Isaya 45 : 24
24 Mmoja ataniambia, Kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.
Yeremia 51 : 10
10 ④ BWANA ameitokeza haki yetu; Njooni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.
Marko 4 : 21
21 Akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango?
Mathayo 5 : 15
15 ⑤ Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Luka 8 : 16
16 Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa mtungi, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.
Marko 5 : 16
16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na kuhusu nguruwe.
Marko 5 : 20
20 Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
Luka 8 : 39
39 Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu.
Luka 12 : 9
9 na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
Mathayo 10 : 32
32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Luka 24 : 48
48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.
Yohana 4 : 30
30 Basi wakatoka mjini, wakamwendea.
Leave a Reply