Biblia inasema nini kuhusu usawa wa rangi – Mistari yote ya Biblia kuhusu usawa wa rangi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia usawa wa rangi

Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.

Matendo 10 : 34 – 35
34 ⑥ Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
35 ⑦ bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.

Warumi 2 : 9 – 11
9 ② dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
10 bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
11 ③ kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

Wakolosai 3 : 11
11 Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.

Yohana 13 : 34
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *