Biblia inasema nini kuhusu usalama wa kanisa – Mistari yote ya Biblia kuhusu usalama wa kanisa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia usalama wa kanisa

1 Mambo ya Nyakati 9 : 21 – 24
21 Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.
22 Hao wote waliochaguliwa kuwa walinzi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyotegemewa kwayo.
23 Basi watu hao na wana wao walikuwa na kazi ya ulinzi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.
24 Hao walinzi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.

Luka 11 : 21
21 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake viko salama;

Nehemia 4 : 10 – 23
10 Lakini Yuda wakasema, Nguvu zao wapagazi zimedhoofika, bado kuna vifusi tele; hatuwezi kuujenga ukuta.
11 Nao adui zetu wakasema, Hawatajua wala kuona, hadi tutakapokuja kati yao, na kuwaua, na kuikomesha kazi hiyo.
12 Kisha Wayahudi waliokaa karibu nao, walikuja, wakatuambia mara kumi: Watakuja kutoka kila sehemu wanapokaa kutushambulia.[5]
13 Basi, nikaweka watu, mahali pa chini pa nafasi iliyokuwa nyuma ya ukuta, mahali palipokuwa wazi, kwa kadiri ya jamaa zao, nikawaweka waliojihami na panga zao, na mikuki yao, na pinde zao.
14 Baada ya kuona haya nilisimama nikawaambia wakuu, maofisa, na watu wengine waliobaki, Msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya, mkawapiganie ndugu zenu, wana wenu, binti zenu, wake zenu, na nyumba zenu.
15 Kisha ikawa, adui zetu waliposikia ya kuwa tumekwisha kupata habari, na ya kuwa Mungu amelibatilisha shauri lao, ndipo sisi sote tukarudi ukutani, kila mtu kwa kazi yake.
16 Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na darii; na viongozi walikuwa nyuma ya nyumba yote ya Yuda.
17 Watu wale walioujenga ukuta, na wale waliochukua mizigo, walijitweka wenyewe, kila mtu alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono wake wa pili alishika silaha yake;
18 nao wajenzi, kila mtu alikuwa na upanga wake, umefungwa ubavuni mwake, ndivyo alivyojenga. Na yeye aliyepiga baragumu alikuwa karibu na mimi.
19 Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wengine; Kazi hii ni nyingi, tena kubwa, nasi tumetawanyika juu ya ukuta, kila mtu akiwa mbali na mwenzake;
20 basi mahali popote mtakaposikia sauti ya baragumu, kimbilieni kwetu; Mungu wetu atatupigania.
21 Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hadi nyota zikatokea.
22 Kadhalika, wakati ule ule, nikawaambia watu, Kila mtu na akae ndani ya Yerusalemu pamoja na mtumishi wake, wapate kuwa walinzi wetu wakati wa usiku, na kufanya kazi wakati wa mchana.
23 Basi mimi, na ndugu zangu, na watumishi wangu, na walinzi waliofuatana nami,[6] hatukuvua nguo zetu hata mmoja; kila mtu alikwenda kuteka maji akichukua silaha yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *