Biblia inasema nini kuhusu urafiki na Mungu – Mistari yote ya Biblia kuhusu urafiki na Mungu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia urafiki na Mungu

Zaburi 63 : 1 – 11
1 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.
3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.
4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Ninakutafakari usiku kucha.
7 Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8 Nafsi yangu inaambatana nawe sana; Mkono wako wa kulia unanitegemeza.
9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza, Wataingia katika vilindi vya nchi.
10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwamwitu.
11 Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Yakobo 4 : 8
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Isaya 65 : 24
24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.

Zaburi 42 : 1 – 2
1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?

Yeremia 31 : 3
3 BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

Yohana 17 : 22 – 23
22 ① Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 ② Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

Wafilipi 3 : 10
10 ⑳ ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

1 Wakorintho 10 : 31
31 ② Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Isaya 55 : 1 – 6
1 ⑮ Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila gharama.
2 Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.
3 ⑯ Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
4 ⑰ Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu.
5 ⑱ Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
6 ⑲ Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu;

Zaburi 139 : 1 – 24
1 ⑰ Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.
2 ⑱ Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
4 ⑲ Maana hamna neno katika ulimini wangu Usilolijua kabisa, BWANA.
5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 ⑳ Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kulia utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17 Mawazo yako ni mazito sana kwangu; Ee Mungu; nayo ni makuu sana.
18 Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe.
19 Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;
20 Wale wanaokusema kwa ubaya, na kutenda maovu juu ya jina lako bure.
21 Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiudhike nao watu wanaokuasi?
22 Nawachukia kwa upepo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu.
23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Kumbukumbu la Torati 6 : 5
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Sefania 3 : 17
17 BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.

Zaburi 51 : 1 – 19
1 Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
3 ① Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4 ② Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 ③ Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanifundisha hekima kwa siri,
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.
10 ④ Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.
11 ⑤ Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12 ⑥ Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya upendo.
13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.
14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
16 Maana hupendezwi na dhabihu, na kama ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19 ⑦ Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng’ombe Juu ya madhabahu yako.

Wakolosai 3 : 1
1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu.

1 Wathesalonike 4 : 3 – 5
3 ⑧ Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 ⑩ kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 ⑪ si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

Yeremia 33 : 3
3 ⑯ Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *