Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia urafiki
Mithali 18 : 24
24 Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Yohana 15 : 13
13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Mhubiri 4 : 9 – 12
9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kupata moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watamstahimili; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
Mithali 27 : 17
17 Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Mithali 17 : 17
17 Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
1 Wathesalonike 5 : 11
11 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.
Mithali 27 : 9
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
1 Wakorintho 15 : 33
33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Waraka kwa Waebrania 10 : 24 – 25
24 ⑪ tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
25 ⑫ wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Mithali 27 : 6
6 Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu.
1 Petro 4 : 8 – 10
8 Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
9 ① Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika;
10 ② kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
Ayubu 6 : 14
14 Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki; Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.
Mithali 22 : 24 – 27
24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;
25 Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.
26 Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu;
27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?
Yohana 15 : 12 – 14
12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
Mithali 27 : 19
19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
Ruthu 1 : 17
17 Pale utakapofia ndipo nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
1 Wakorintho 13 : 1 – 13
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
1 Samweli 22 : 23
23 ④ Kaa wewe pamoja nami, usiogope; kwa maana yeye atafutaye roho yangu, ndiye atafutaye na roho yako; nawe utakaa kwangu salama.
Mithali 17 : 9
9 Afunikaye kosa hutafuta kupendwa; Bali yeye afichuaye siri hutenga rafiki.
Leave a Reply