Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upinde
Mwanzo 21 : 16
16 ⑫ Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
Mwanzo 21 : 20
20 ⑯ Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
2 Samweli 22 : 35
35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu inaupanda upinde wa shaba.
Ayubu 20 : 24
24 ⑰ Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma.
Zaburi 18 : 34
34 Anaifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.
Ezekieli 39 : 9
9 Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;
Isaya 13 : 18
18 Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.
Maombolezo 2 : 4
4 Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto.
Ezekieli 39 : 3
3 nami nitaupiga upinde wako, utoke katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako nitaiangusha, itoke katika mkono wako wa kulia.
Yeremia 49 : 35
35 ③ BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama nitauvunja upinde wa Elamu, ulio mkuu katika nguvu zao.
Mwanzo 49 : 24
24 ① Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli,
Ayubu 16 : 13
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua figo zangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.
Ayubu 29 : 20
20 ⑥ Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejeshwa upya mkononi mwangu.
Zaburi 78 : 57
57 ⑬ Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakayumba kama upinde usiofaa.
Maombolezo 3 : 12
12 ⑰ Ameupinda upinde wake, Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.
Leave a Reply