Biblia inasema nini kuhusu Upepo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Upepo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upepo

2 Wafalme 19 : 7
7 Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.

2 Wafalme 19 : 35
35 ① Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia moja themanini na tano elfu. Na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.

Mwanzo 41 : 6
6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

Ezekieli 19 : 12
12 Lakini aling’olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila.

Hosea 13 : 15
15 Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya BWANA itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.

Luka 12 : 55
55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

Yona 4 : 8
8 Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akatayarisha upepo wa mashariki, wenye joto jingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.

Ayubu 27 : 21
21 Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake.

Kutoka 10 : 19
19 BWANA akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.

Mithali 25 : 23
23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.

Ayubu 37 : 17
17 Jinsi nguo zako zilivyo na moto, Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini?

Ayubu 37 : 9
9 Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake.

Ayubu 37 : 21
21 Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung’aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa.

Hosea 4 : 19
19 Upepo umemfunika kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao.

Yeremia 22 : 22
22 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *