Biblia inasema nini kuhusu Upendo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Upendo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upendo

Kutoka 20 : 6
6 ⑱ nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kumbukumbu la Torati 5 : 10
10 ② nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kumbukumbu la Torati 6 : 5
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Kumbukumbu la Torati 7 : 9
9 Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hadi vizazi elfu;

Kumbukumbu la Torati 10 : 12
12 ⑤ Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;

Kumbukumbu la Torati 11 : 1
1 ⑭ Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake.

Kumbukumbu la Torati 13 : 3
3 ⑲ wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.

Kumbukumbu la Torati 30 : 6
6 BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.

Kumbukumbu la Torati 30 : 16
16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 30 : 20
20 ② kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

Yoshua 22 : 5
5 ⑫ Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.

Kumbukumbu la Torati 11 : 13
13 Tena itakuwa, mtakapoyazingatia kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,

Kumbukumbu la Torati 11 : 22
22 Kwa kuwa kama mtayazingatia kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;

Yoshua 23 : 11
11 Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.

Zaburi 18 : 1
1 ⑦ Wewe, BWANA, nguvu yangu, nakupenda sana;

Zaburi 31 : 23
23 Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.

Zaburi 37 : 4
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.

Zaburi 45 : 11
11 ⑪ Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.

Zaburi 63 : 6
6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Ninakutafakari usiku kucha.

Zaburi 69 : 36
36 Wazawa wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.

Zaburi 73 : 26
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.

Zaburi 91 : 14
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

Zaburi 97 : 10
10 ⑯ Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

Zaburi 116 : 1
1 Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *