Biblia inasema nini kuhusu Upako – Mistari yote ya Biblia kuhusu Upako

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upako

Kumbukumbu la Torati 28 : 40
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.

Ruthu 3 : 3
3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; lakini usijioneshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.

Esta 2 : 12
12 Basi zamu ya kila mwanamwali kuingia kwa mfalme Ahasuero, iliwadia baada ya kutayarishwa kulingana na sheria ya wanawake kwa miezi kumi na miwili; kwa kuwa ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;

Zaburi 92 : 10
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.

Zaburi 104 : 15
15 Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.

Zaburi 141 : 5
5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.

Mithali 27 : 9
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.

Mithali 27 : 16
16 Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kulia hukuta mafuta.

Mhubiri 9 : 8
8 Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose manukato.

Wimbo ulio Bora 1 : 3
3 Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.

Wimbo ulio Bora 4 : 10
10 Jinsi pendo lako lilivyo nzuri, dada yangu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.

Isaya 57 : 9
9 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hadi kuzimu.

Amosi 6 : 6
6 ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu.

Mika 6 : 15
15 Utapanda, lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 15
15 Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wale wote waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.

Luka 7 : 46
46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.

Isaya 1 : 6
6 Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.

Marko 6 : 13
13 ⑯ Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya.

Luka 10 : 34
34 akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

Yakobo 5 : 14
14 Mtu wa kwenu amekuwa mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

Ufunuo 3 : 18
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Mathayo 26 : 12
12 Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.

Marko 14 : 8
8 Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.

Marko 16 : 1
1 Na sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

Luka 23 : 56
56 ⑭ Wakarudi, wakatayarisha manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *