Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uovu
Mwanzo 3 : 15
15 ⑱ nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Mambo ya Walawi 19 : 14
14 ⑱ Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.
Mambo ya Walawi 19 : 18
18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.
Kumbukumbu la Torati 27 : 18
18 ⑪ Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 32 : 33
33 Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka.
2 Wafalme 6 : 22
22 Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.
Ayubu 31 : 30
30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
Zaburi 4 : 2
2 Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?
Zaburi 7 : 16
16 ⑮ Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.
Ayubu 15 : 35
35 Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Na mioyo yao hutunga udanganyifu.
Zaburi 10 : 10
10 Hujikunyata na kuinama; Watu duni huanguka kwa nguvu zake.
Zaburi 10 : 14
14 Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
Zaburi 21 : 11
11 Wakipanga kukutenda mabaya, Kwa miango ya hila, hawatafanikiwa.
Zaburi 22 : 8
8 ⑩ Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.
Zaburi 35 : 16
16 Bila heshima walinidhihaki kupindukia, Wakanisagia meno yao.
Zaburi 35 : 21
21 Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.
Zaburi 38 : 16
16 Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.
Zaburi 38 : 19
19 Lakini walio adui zangu bila sababu wana nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.
Zaburi 41 : 8
8 Wanafikiri pigo liualo limemshika, Akalala asiweze kusimama tena.
Zaburi 55 : 3
3 Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.
Zaburi 55 : 11
11 Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.
Zaburi 56 : 6
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa waliniotea ili waniue.
Zaburi 57 : 4
4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Zaburi 57 : 6
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Zaburi 59 : 4
4 Bila kosa langu wanaenda mbio, kujiweka tayari; Inuka utazame na kunisaidia.
Zaburi 59 : 7
7 Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?
Zaburi 62 : 4
4 Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.
Zaburi 64 : 1 – 168
1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
2 Unifiche mbali na njama za watenda mabaya, Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu;
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Wakisema, Ni nani atakayeiona?
6 Ni nani atambuaye maovu yetu? Tumepanga njama kwa werevu mwingi, Maana katika moyo wa mtu na fikira mengi yamefichika.[9]
7 Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake, Na kuwajeruhi ghafla.
8 Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa; Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake.
10 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watasifu.
Leave a Reply