Biblia inasema nini kuhusu Uoga – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uoga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uoga

Mambo ya Walawi 26 : 37
37 ⑩ Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu.

Kumbukumbu la Torati 20 : 8
8 Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.

Kumbukumbu la Torati 32 : 30
30 Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?

Yoshua 7 : 5
5 ⑮ Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye materemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.

Yoshua 23 : 10
10 Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.

Waamuzi 7 : 3
3 ③ Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu yeyote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu elfu ishirini na mbili wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.

Ayubu 15 : 24
24 Mateso na dhiki humtia hofu; Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;

Ayubu 18 : 11
11 Vitisho vitamtia hofu kutoka kila upande, Na kumfukuza karibu na visigino vyake.

Mithali 28 : 1
1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

Mithali 29 : 25
25 ⑯ Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Isaya 51 : 13
13 ⑱ Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?

Wagalatia 6 : 12
12 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.

Mwanzo 3 : 12
12 ⑮ Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

Mwanzo 12 : 19
19 Mbona ulisema, Huyo ni dada yangu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako.

Mwanzo 20 : 12
12 Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.

Mwanzo 26 : 9
9 Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni dada yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nilisema, Nisife kwa ajili yake.

Mwanzo 31 : 31
31 Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Kwa sababu niliogopa, nikasema, Usije ukaninyang’anya binti zako kwa nguvu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *