Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia unywaji wa kijamii
Mithali 20 : 1
1 ③ Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
Waefeso 5 : 18
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
Wagalatia 5 : 21
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Isaya 5 : 22
22 Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, na walio hodari wa kuchanganya vileo;
Habakuki 2 : 15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
1 Petro 5 : 8
8 ⑲ Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Mithali 23 : 29 – 35
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31 Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
1 Wakorintho 5 : 11
11 ⑤ Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Luka 21 : 34
34 Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
1 Timotheo 3 : 3
3 asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
Isaya 5 : 11
11 ⑰ Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Kumbukumbu la Torati 14 : 26
26 na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Mathayo 15 : 11
11 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Mathayo 6 : 33
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
1 Petro 4 : 3
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu;
1 Wakorintho 8 : 9
9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.
Luka 7 : 33 – 35
33 ⑧ Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo.
34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.
35 Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Leave a Reply