Biblia inasema nini kuhusu unyenyekevu – Mistari yote ya Biblia kuhusu unyenyekevu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia unyenyekevu

Yakobo 4 : 6
6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

Wafilipi 2 : 3 – 11
3 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuko na namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Luka 14 : 11
11 Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

1 Petro 5 : 6
6 ⑰ Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;

Mithali 22 : 4
4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.

Wakolosai 3 : 12
12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

Mathayo 23 : 12
12 ⑫ Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.

Warumi 12 : 3
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

1 Petro 5 : 5
5 ⑯ Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

Yohana 3 : 30
30 ④ Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.

Yeremia 9 : 23
23 ⑯ BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

Yakobo 4 : 10
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

Waefeso 4 : 2
2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;

Marko 9 : 33 – 37
33 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?
34 Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.
35 Akaketi chini, akawaita wale Kumi na Wawili akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
36 Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia,
37 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

2 Wakorintho 12 : 5 – 12
5 Kuhusu mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.
6 Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
8 Kwa ajili ya kitu hicho nilimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.
9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na matusi, na matatizo, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
11 Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.
12 Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika subira yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.

Mithali 11 : 2
2 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.

Zaburi 131 : 1
1 ⑫ BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.

Warumi 11 : 18
18 ⑫ usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.

2 Wakorintho 11 : 30
30 Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.

Mithali 18 : 12
12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *