Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Umeme
Ayubu 28 : 26
26 Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.
Ayubu 37 : 3
3 Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi.
Ayubu 38 : 25
25 Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;
Ayubu 38 : 35
35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
Zaburi 18 : 14
14 ⑰ Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya.
Zaburi 77 : 18
18 Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;
Zaburi 78 : 48
48 Akaacha ng’ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe, Na makundi yao kwa umeme.
Zaburi 97 : 4
4 Umeme wake uliuangaza ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka.
Zaburi 135 : 7
7 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.
Zaburi 144 : 6
6 Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
Yeremia 10 : 13
13 Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.
Yeremia 51 : 16
16 ⑪ Atoapo sauti yake pana kishindo cha maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.
Ezekieli 1 : 14
14 Na wale viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme.
Danieli 10 : 6
6 ③ mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.
Nahumu 2 : 4
4 Magari ya vita yanafanya vishindo njiani, Yanasonganasongana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.
Zekaria 9 : 14
14 Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.
Zekaria 10 : 1
1 ⑰ Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.
Mathayo 24 : 27
27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Mathayo 28 : 3
3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.
Luka 10 : 18
18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
Ufunuo 4 : 5
5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Ufunuo 8 : 5
5 Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.
Ufunuo 11 : 19
19 Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.
Ufunuo 16 : 18
18 ⑫ Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
Leave a Reply