Biblia inasema nini kuhusu ulimi – Mistari yote ya Biblia kuhusu ulimi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ulimi

Mithali 12 : 18
18 Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.

1 Petro 3 : 10
10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme uongo.

Mithali 21 : 23
23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.

Mithali 18 : 21
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

Yakobo 3 : 8
8 ⑮ Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Yakobo 3 : 6
6 ⑭ Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.

Yakobo 1 : 26
26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

Mambo ya Walawi 19 : 16
16 ⑳ Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu[9] ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.

Yakobo 3 : 5
5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

Yakobo 3 : 1 – 18
1 ⑫ Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
2 ⑬ Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili watutii, hivi twageuza mwili wao wote.
4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, kokote anakoazimia kwenda nahodha.
5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 ⑭ Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8 ⑮ Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 ⑯ Kwa huo tunamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo unwawalaani wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.
13 ⑰ Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
14 ⑱ Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
15 ⑲ Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya kidunia, ya tabia ya kibinadamu, na ya kishetani.
16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
17 ⑳ Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

Zaburi 12 : 3 – 4
3 BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi;
4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?

Waefeso 4 : 29
29 ⑮ Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Mithali 20 : 19
19 Mwenye udaku hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *